Uungu wa Yesu

Watu wengi hutangaza hadharani kwamba Yesu ni Mungu hali hiyo hutokana na mtu kutokuwa na Elimu ya kutosha kuhusu chanzo cha Yesu kuitwa Mungu katika nafsi ya Pili. Ndani ya makala hii nitaeleza kwa undani Uungu huo wa Yesu ilivyoanza Insha’Allah.

MASLAHI ya Dunia hii yamewafanya watu wengi wenye elimu kuhusu Yesu kuwa Mungu washindwe kuwaeleza watu ukweli kuhusu Umungu wa Yesu wameamua kuwadanganya makusudi.

Siri zilizomo Kanisani ambazo zinamzuwiya Kiongozi kuwafundisha watu ukweli na nidhamu ya woga iliyojengwa ndani ya Wafuasi inamfanya mtu akubali jambo bila kulielewa kabisa akiuliza husomewa Yohana 1:1-5 na kupewa tafsiri potofu lazima akubaliane na Kiongozi wake hiyo ndiyo Sera ya kudanganya watu na kweli wamedanganyika kama unavyowaona ukimwambia ukweli yuko tayari kupigana na kuuwa mtu, hata hivyo lazima ukweli tuuseme tu kwa kumuogopa Mungu. Mathayo 10 :26-27.

Kwa kuzingatia umuhimu wa somo hili inabidi tuligawe katika sehemu Nne ili kupata ushahidi wa fundisho la imani ya utatu wa Mungu mmoja. Sehemu hizo ni kama ifuatavyo: -

*Matamshi ya Yesu mwenyewe kuhusu Uungu wake. Anasemaje?
*Wanafunzi wa kwanza wa Bwana Yesu walimfahamu kwamba ni Mungu au vipi?
*Maaskofu waliofuata baada ya wanafunzi wa kwanza tangu Karne ya kwanza hadi karne ya tatu je? Walifundisha vipi kuhusu Yesu.
*Imani ya utatu ilivyoanza hadi kuwa fundisho kamili na kanuni ya Wakristo Duniani pote.

Yesu anasemaje katika Injili yake:
Yohana 17:3 imeandikwa hivi –
uzima wa milele ndiyo huu wakujue Mungu wa pekee na Yesu uliyemtuma.
Katika Aya hii Yesu anasema kwamba ili kupata uzima lazima tumjue kwanza Mungu wa pekee na umjue Yesu Kristo aliyetumwa na Mungu, hapa Yesu hasemi lolote kuhusu yeye kuwa nafasi ya pili ya Mungu ila anakiri wazi yeye ametumwa na Mungu mmoja wa pekee.

Luka 2:40 imeandikwa hivi: -
Yule mtoto akakua akaongezeka nguvu amejaa hekima na neema ya Mungu ilikua juu yake.

Katika Aya hii tunaambiwa kwamba Yesu alijaa hekima na neema ya Mungu. Tahadhari ufikirie vizuri kwa makini sababu hapa inayonyesha kwamba bila ya Mungu kumpa neema Yesu asingelikuwa na hekima hii inaonyesha wazi Yesu ni kiumbe aliyeteuliwa na Mungu na hii ni kawaida yake Mwenyezi Mungu kwa Mitume na Manabii wake kuwapa neema na hekima.

Yohana 13:13 imeandikwa hivi: - Nanyi mwaniita Mwalimu na Bwana nanyi mwasema vema maana ndivyo nilivyo. Maneno hayo yatueleza wazi kwamba alikuwa anajua wazi kwamba yeye ni Mwalimu na Bwana ndiyo maana anawasifu wanafunzi wake, NANYI MWASEMA VEMA.

Mathayo 23:9 imeandikwa: - Wala msimwite mtu Baba maana Baba yenu ni mmoja wa Mbinguni wala msiitwe Kiongozi maana Kiongozi wenu ni mmoja naye ndiye Yesu Kristo. Hapa Yesu anaendelea kutuonyesha jinsi alivyo tofauti na Mungu, na yeye hayuko sawa na Mungu daima Mungu ni Baba lakini Yesu ni Kiongozi tu.

Ufunuo: 1:1-2 imeandikwa hivi: - Ufunuo wa Yesu Kristo aliopewa na Mungu awaonyeshe watu wake…Naye akatuma Malaika akamuonyeshe Mtumwa wake Yohana… Wakati ufunuo unatolewa na Mungu na kupewa Yesu wakati huo Yesu ameshatoka Duniani yuko Mbinguni (kwa mujibu wa bible), lakini bado inaonyesha Mungu ndiye mkubwa Yesu bado ni wakutumwa ili awaonyeshe watumwa kuhusu mambo yao yatakayokuja kama tulivyosoma. Zipo Aya nyingi sana zinazoonyesha wazi kuwa Yesu alikuwa halijui kabisa fundisho la tatu na wala kuhusu kuwa yeye ni Mungu.

Wanafunzi wa kwanza walimuelewaje Yesu?
Matendo ya Mitume 3:13 imeandikwa hivi… Mungu wa Ibrahimu na wa Isaka na wa Yakobo, Mungu wa Baba zetu amemtukuza Mtumishi wake Yesu ambaye nyinyi mlimsaliti na kumkana mbele ya Pilato, alipokuwa ametoa hukumu yake ili afunguliwe.

Maneno ya wanafunzi yalikuwa wazi kuwa Yesu ni Mtumishi wa Mungu tu yaani Mtume pia ni Nabii.
Matendo ya Mitume 4:27 imeandikwa hivi… maana ni kweli Herode na Pontio Pilato pamoja na Mataifa na watu wa Israel walikusanyika katika mji huu juu ya Mtumishi wako Mtakatifu Yesu uliyemtia mafuta. Wanafunzi wanaendelea na msimamo wao kwamba Yesu ni Mtumishi wa Mungu aliyetumwa (Mtume) tu. Luka 24:19 imeandikwa: - …Akawauliza mambo gani? Wakamwambia mambo ya Yesu Wanazareti aliyekuwa mtu nabii mwenye uwezo wa kutenda na kusema mbele za Mungu na Wanadamu.

Marko 6:2 imeandikwa: - Na ilipokuwa Sabato aliingia katika Sinagogi, wengi waliposikia walishangaa wakasema huyu ameyapata wapi haya! Hekima gani hii? Aliyopewa huyu? Nini miujiza hii mikubwa inayotendeka kwa mikono yake? Huyu si ni yule Selemala mwana wa Mariamu na nduguyao Yakobo na Yosef na Yuda na Simoni na Maumbu wake hawapo hapa? (Maana ya Umbu ni dada)
Maneno haya yanathibitisha kwamba watu waliomfahamu Yesu walishangaa matendo makubwa anayoyatenda hata hivyo walijua kwamba yeye ni Selemala wa Mwana wa Mariamu tu. Na ni kiumbe mwenye ndugu zake na dada zake, kama watu wengine.

Marko 13:31 tunasoma hivi – Mbingu na Nchi zitapita lakini maneno yangu hayatapita kamwe. Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna anaye ijua hata malaika wala Mwana (Yesu) ila Baba tu Mungu… Hapa Yesu alikua anazungumza habari ya siku ya mwisho alikiri wazi kwamba yeye siku haijui hata Malaika hawajui ila Mungu peke yake.

Baadhi ya Maaskofu wa mwanzoni wanasemaje kuhusu Yesu: -
Justin Martyr: Alimtaja Yesu kwamba hakuwa Binadamu alikua Malaika aliyeumba… Yesu alikua na cheo kidogo kuliko Mungu... Justin aliuwawa mjini Rome mwaka 165 A.D. kwa kukatwa kichwa.
Irenayo. Alifundisha kwamba Mungu ni mmoja wa pekee hakuna tena mwingine wa kulingana naye…Yesu aliumbwa kama Malaika hayuko sawa na Mungu. Ilikuwa mwaka 200 A.D.
Naye Clement, wa Alexandaria. Alifundisha kwamba Mungu ni mmoja tu wa kweli asiyeumbwa na hawezi kuangamiaYesu ni wa pili lakini hayuko sawa na Mungu. Clement alikufa mwaka 215 AD.
Askofu Mkuu Tertuliano: Alifundisha kwamba Mungu ni mkubwa kuliko vyote. anayetumwa ni mdogo kwa yule anayemtuma. Yesu alitumwa na Mungu alifundisha hivyo mwaka 230 AD.
Askofu Hippolytus. Alifundisha kwamba Mungu ni mmoja wa pekee, Muumba wa vyote hakuna tena kilichomtangulia. Na Yesu aliumbwa na Mungu. Askofu Hippolytus inasemakana alikufa mwaka 235 AD. Kwa kuvutwa huku na huku na kuchanika vipande viwili. Wauwaji walitumia farasi kumvuta muanga huyu.
Naye Askofu Origen. Alifundisha kwamba Baba Mwana ni asili mbili tofauti ukilinganisha na Baba Mwana Yesu anayo nuru ndogo sana mbele za Baba. Askofu huyu aliishi kati ya mwaka 185-254 AD.

Ndugu msomaji baada ya kumsikiliza Yesu katika Injili yake katika Aya nilizotoa hatukuona Neno linalosema yeye ni Mungu hata kidokezo kidogo hakuna. Baadaye tumewasikia wanafunzi wake wa kwanza waliotembea na Yesu pia hawakutuambia kwamba Yesu ni Mungu tumeona wakitaja kwamba. Yesu ni Mtume, Mwalimu, Nabii, mtiwa mafuta, Bwana, mtu, Selemala, na Mwana wa Mariamu na yeye mwenyewe alipenda kujiita Mwana wa adam tu. Kama tulivyoona Maaskofu wa kwanza nao hawakutuambia wazi kwamba Yesu ni Mungu au Roho Mtakatifu ni Mungu kufika hapa ndugu msomaji unaweza kuuliza sasa fundisho hili kubwa na ndiyo kanuni ya Wakristo lilianza vipi? Hadi kuwa ndiyo imani kuu namna hiyo? Je? Ni mpango wa Mungu kweli? Naomba uendelee kusoma.

Uungu wa Yesu ulianza vipi?
Tangu mwishoni mwa Karne ya tatu ulitokea mvutano mkubwa sana katika Kanisa kuhusu mafundisho ya Maaskofu kuhusu Cheo cha Yesu na Mariamu. Mabishano hayo yaliendelea kwa kasi kila mtu alimtafsiri Yesu kivyake. Hali ilizidi kuwa mbaya sana mpaka mnamo mwaka 325 AD ilimlazimu Mfalme wa wakati huo Konstantine awaite Maaskofu wote wa wakati huo, inasemekana Maaskofu walio udhuria ni kati ya 250-318 ili waje waelewane na kuwa na msimamo mmoja lakini ni sehemu tu ya Maaskofu walio hudhuria. Wakati huo Konstantine alikuwa Mpagani mwabudu jua kwa wazazi wake, (soma kitabu kinachoitwa The Early Church). Aliwakusanya Maaskofu ili kuleta utulivu katika utawala wake. Mfalme huyu ndiye aliyekuwa Mwenyekiti na mtendaji muhimu katika mkutano huo. Majadiliano yalikuwa makali sana iliwachukua miezi miwili bila mwafaka wowote ndipo Mfalme aliingilia kati na kutoa uamuzi wake na ndiyo uliofuatwa. Yeye aliwaunga mkono wale waliosema Yesu ni Mungu kweli na ni mtu kweli pia ni mwana wa Mungu aliye sawa na Baba yake Mungu, pia Mariamu ni mama wa Mungu pia ni Malkia wa Mbinguni. Kwa hiyo Mfalme Mpagani aliyekuwa bado mwenye imani za kipagani akawa ameshiriki sehemu ya maana sana katika kumpandisha cheo Bwana Yesu toka kuwa mtume hadi kuwa Mungu kamili na Mariamu akawa mama wa Mungu. Kama nilivyosema Kostantini alikuwa Mpagani hivyo, hakuwa na ujuzi kamili juu ya maswali yaliyokuwa yakiulizwa katika Thiolojia ya Kigiriki alilojua ni kuleta amani katika utawala wake tu. (Soma A Short History of Christian Doctrine).
Uamuzi huo ulikuwa ni wa kijeshi na si hiyari, na Maaskofu waliomhofu Mfalme, baadhi walitia sahihi zao lakini wengine walikataa, (baadhi ya kikundi kilicho kataa ni kile kilicho julikana kama Arian) waliokataa waliteswa sana na kunyanyaswa, kuna waliuwawa kikatili kwa kuchomwa moto wakiwa hai na mateso mengine kadhaa wa kadha yasiyo semekana. (Theologian Arius 250-336 AD, who lived and taught in Alexandria, Egypt, in the early 4th century). Mkutano huo ulikuwa katika mji wa NICEA na uliitwa Baraza la NICEA mwaka 325 AD. The First Council of Nicaea 325 C uwamuzi wa NICEA haukuleta utulivu kama ulivyotegemewa, bali ulisababisha vurugu za hali ya juu, mateso na mauaji yalikuwa makubwa sana hasa kwa wale waliokataa fundisho hilo la Yesu kuwa Mungu na Mariamu kuwa mama wa Mungu, Malkia na Mbinguni. (Sophia) Mateso na mabishano yalienea zaidi huko Ufaransa ya Kusini, Hispania na Ujerumani miaka mingi iliyopita hasa baada ya Patano la Milano ambapo Kostantini na Kanisa walishirikiana vizuri. Makanisa yakajengwa kwa gharama za serikali na hapo mateso yalizidi, watu wengi waliuwawa vibaya na hovyohovyo tu bila kuangalia haki za binadam. Ilifikia kipindi hata baadhi ya watu kuokwa kwenye matanuri ya moto. (Soma kitabu kinachoitwa Jesus and the Goddess by Timothy Freke & Peter gandy)Ilipofika mwaka 381 A.D. mambo yalizidi kuwa mabaya sana, hapo Mfalme aliyekuwa anatawala wakati huo Theodosius aliitisha tena mkutano wa Maaskofu wote. Katika mkutano huo Mfalme alitangaza rasmi kuunga mkono uamuzi wa Baraza la NICEA.

Pia walikubaliana Roho Mtakatifu aunganishwe katika utatu Mtakatifu hapo ndipo imani ya utatu wa Mungu Mmoja ilianza ili kuwathibiti wale waliokuwa wanapinga ilitolewa amri kwamba hakuna ruksa kwa mtu yeyote kupinga au kutafsiri neno linalohusu Biblia au mapokeo soma Hati ya Ufunuo ya Vaticani 10:4 imeandikwa: -
Lakini haki ya kutoa tafsiri thabiti ya neno la Mungu au mapokeo imekabidhiwa mamlaka ya kifundishi ya Kanisa Katoliki peke yake tu. Mkutano huo unaitwa Baraza la Kostantinopol. Mwaka 381 A.D. Historia inaendelea kutueleza kwamba Kanisa liliendelea kuwatesa na kuwauwa wote waliojaribu kupinga au kufafanua vingine, mamlaka ya Kanisa ikishirikiana na serikali, watu waliteswa kwa njia nyingi, mfano: -
wapo waliofungwa na kunyimwa chakula hadi kufa, wengine walitupwa kwenye zizi lililokuwa na wanyama wakali na kuliwa na wengine walilazimishwa kukalia vyuma vyenye moto, wengine walivalishwa shingoni mikufu yenye misumari yenye ncha kali baadaye misumari ilipigiliwa na kuingia shingoni hadi kufa. Wengine walibanwa na Koleo maalum Magotini na kuvunja miguu na kuwalazimisha wakubali mafundisho ya Kanisa la Roma. Wapo waliochunwa ngozi ya mwili wakiwa hai mfano wa mbuzi na walikufa kwa mateso makali.

Uamuzi huu wakutisha ulikuwa unatimiza maneno ya Yesu Mathayo 12:36. Nawaambia hakika, siku ya hukumu watu watatakiwa kujieleza kuhusu kila neno lisilo la maana walilolisema. Vile vile Yesu anasema… Mathayo 13:36-43 ...Akasema azipandaye mbegu njema ni mwana wa Adamu lile Konde ni ulimwengu zile mbegu njema ni wana wa Mfalme, yale magugu ni wana wa yule mwovu aliyepanda ni Ibilisi mavuno ni mwisho wa dunia wavunao ni malaika kama vile magugu yanavyokusanywa na kuchomwa motoni ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa Dunia… mwenye masikio na asikie.

Uamuzi huo ulitimiza kweli magugu yalikuwa yamepandwa Ulimwenguni, imani ya uongo iliingia kwa nguvu kama vile magugu yanavyoingia shambani na kuharibu ngano. Ndivyo ilivyo hadi leo hii fundisho hilo la uongo limekuwa ndiyo msingi mkubwa wa imani ya Kanisa Duniani pote. Ipo njia inayoonekana kuwa sawa machoni mwa mtu lakini mwisho wake ni mauti mithili 14:12 Viongozi wa Kanisa waliona kwamba njia nzuri ya kumuheshimu Yesu ni kumpandisha Cheo toka Mtume wa Mungu hadi kuwa Mungu sawa Mungu Muumba vyote kabisa. Mariamu akapandishwa kutoka mama wa Mtume Mtakatifu. Viongozi wakampandisha cheo cha mama wa Mungu na ni Malkia wa Mbinguni!!! Viongozi hao inafaa wafungwe jiwe la kusagia shingoni sababu wamewakosesha watu hadi leo hii wanaendelea kuwakosesha kwa mafundisho ya uongo Marko 9:42. Ndugu Msomaji ninakushauri uende Maktaba utaona vitabu na kurasa maelfu ambavyo wanathiolojia wamejitahidi sana kutoa fafanuzi mbalimbali na mitajo ya kila aina ili kupata ukweli wa mambo kuhusu utatu lakini huishia kuchanganyikiwa, na kuacha bila kuelewa na hawapati ushahidi ulio yakinifu. Baadhi ya Wanatheolojia wanasemaje?
Kitabu cha A Short History of Christian Doctrine. Mwanathiolojia Bernhard Lohse anaeleza kwamba …ingawa Agano Jipya linahusika sana hata hivyo hatupati fundisho la utatu katika Agano Jipya.
Kitabu cha New International Dictionary of New Testament Theology, kinasema
…hakuna kabisa ushahidi katika Agano Jipya unaothibitisha utatu.
Profesa wa Chuo Kikuu cha Yale bwana E. Washburn Hopkins anasema katika kitabu cha Origin and Evolution of Religion kwamba …hata Yesu mwenyewe halijui kabisa fundisho hilo la utatu sababu hakuna mtajo popote unaotuambia kwamba yeye ni Mungu. Dhana hii ya utatu ilikuja miaka mia tatu baada ya kuondoka bwana Yesu.
Mwana Historia Weigall, Arthur anasema katika kitabu cha The Paganism in our Christianity …kwamba wazo la utatu liliingizwa na viongozi wa kanisa mnamo karne ya tatu baada ya kuondoka bwana wetu…Vitabu vyote vya Agano la kale na Injili zote nne hakuna fundisho hilo kabisa kama linavyofundishwa makanisani duniani pote siku hizi.
Kitabu cha New Catholic Encyclopaedia tunapata maelezo kwamba mamlaka ya Kanisa husema wazi kwamba ...utatu siyo fundisho la moja kwa moja…ila ni fumbo la imani tu.
Kitabu cha Kikatoliki Trinitas A. Thiolojicar Encyclopandia of the Holy Trinity Tertuliano. Baadhi ya mafundisho yake yalitumiwa na watu wengine…na hutahadharisha kutokua na haraka kuhusu utatu.
Katika vitabu vya New Catholic Encyclopadia na The Encyclopadia of Religion wanathiolojia hukubaliana kwamba katika Biblia hakuna fundisho la utatu… kabisa.
Mwanathiolojia Myeswiti Edmund Fortiman anatueleza katika kitabu cha The Triune God kwamba …katika Agano la Kale hatuoni ushahidi wa mwandishi mtakatifu yeyote anayetuambia lolote kuhusu utatu… uchunguzi wa maandiko Matakatifu ya kiebrania umeonyesha kwamba hakuna fundisho la ajabu jinsi hiyo katika Biblia.
Kitabu cha Encyclopadia Americana kinasema kwamba imani ya utatu lilikuwa fundisho la upotevu tangu Karne ya nne na ni upagani.

Baada ya kupitishwa uamuzi huo Historia, inatuonyesha kwamba fundisho hilo halikupokelewa kama ilivyotarajiwa watu waliendelea kupinga sana hata hivyo waliopinga waliteswa, kudhalilishwa, mateso haya yaliongozwa na Kanisa lenyewe.Na baada ya karne nyingi utatu ulipangwa imara sana, kitabu cha The Encyclopadia Americana kinatueleza kwamba imani ya utatu ilianza magharibi katika mifumo ya kinadharia ya wanachuo katika enzi za katikati ambapo ufafanuzi ulianza kutolewa kwa namna ya Falsafa na Saikolojia. Historia inaendelea kutudokeza kwamba imani ya utatu haikujulikana katika Kanisa la Mashariki mpaka Karne ya 12 (The Encyclopadia Britanica) hadi karne ya 17 inaonekana kwamba imani hiyo ilitungwa kusini mwa Ufaransa karne ya 5 sababu inaonyesha kwamba mvutano mkubwa ulikuwa Kusini mwa Ufaransa na Hispania na katika karne 6 – 7 ilitumiwa katika Liturjia ya Kanisa Ujerumani ilianza kutumiwa Luturjia ya utatu karne ya 9 na baadaye kidogo ilianza kutumiwa Roma. Kwa maana hiyo fundisho la utatu lilichukua miaka mingi sana tangu lipitishwe hadi kukubaliwa na watu wengi. Naye E. W. Hopkins anasema katika kitabu cha Origin and Evolution of Religion. Misimamo ya fundisho la utatu ililenga hasa katika Siasa ya Kanisa tu, siyo fundisho la kweli. Baada ya uamuzi kupitishwa kilichofuata ni utekelezaji jambo ambalo lilikuwa gumu sana. Ukisoma A Dictionary of Religions Knowledge inasema kwamba, Wanautatu hawaafikiani wao kwa wao wenyewe kuhusu fundisho hilo la utatu jinsi linavyopaswa kufafanuliwa. New Catholic Encyclopaedia kinasema ni walimu wachache wa Thiolojia ambao huwa hawasumbuliwi na maswali wanapofundisha katika Seminari za Kiroma. Lakini mtu anawezaje kuhubiri kuhusu utatu? Na iwapo swali hilo ni dalili za mvurugiko kwa wanafunzi basi ni dadili ya mvurugiko hata kwa Maprofesa wao. Naye Myeswiti Joseph A. Bracken anatueleza kwamba Mapadri ambao kwa bidii sana miaka mingi wawapo Seminary hujifunza utatu… husita kuufundisha siku za Jumapili soma What Are They Saying About the Trinity, kwa nini mtu achoshe watu akili kwa fundisho ambalo hawawezi kulielewa? …tofauti zinazofundishwa kuhusu utatu haziwezi kutosheleza kumfanya binadam aelewe mitajo ya Kitheolojia iliyotokana na Kisiria, Kigiriki na Kilatini humfanya mtu, kuuona huo ni upuuzi na mchezo wa maneno …kwanini mtu aongeze kitu katika upweke wa Mwenyezi Mungu Muumba wa vyote?

Mwisho napenda kumnukuu Father John L. Mackenzie, yeye anasema hivi:
"U'tawa uliotegemezwa juu ya makosa huwezi kuutetea."